Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi na Awali Wilaya ya Hanang, Geofrey Abayo, amekutana na Maafisa Elimu wa kata zote kwa lengo la kuweka mikakati thabiti ya kuinua kiwango cha elimu katika shule za msingi na awali wilayani hapa.
Kikao hicho, kilichofanyika Mei 30, 2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’, kiliangazia kwa kina masuala ya msingi yanayochangia kupanda au kushuka kwa ubora wa elimu, ikiwemo ufaulu wa wanafunzi, nidhamu, na changamoto ya utoro mashuleni.
Akizungumza kwenye kikao hicho, Abayo alisisitiza umuhimu wa kuimarisha usimamizi shuleni na kuhakikisha mazingira rafiki ya kujifunzia na kufundishia yanakuwepo ili kusaidia kuinua viwango vya elimu.
Maafisa elimu kwa upande wao waliunga mkono maelekezo yaliyotolewa na kuahidi kuyatekeleza kwa vitendo katika maeneo yao, kwa lengo la kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta ya elimu.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: +255 762 362 950
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.