Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Teresia Irafay, leo Mei 20, 2025 amekutana na kufanya kikao maalum na watumishi wote wa mkataba wa halmashauri hiyo kwa lengo la kusikiliza na kujadili changamoto zinazowakabili.
Katika mkutano kikao uliojaa usikivu na uwazi, Irafay ameelezea juu ya baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo watumishi hao, huku akisisitiza umuhimu wa kushughulikia stahiki zao kwa wakati ili kuongeza ari ya utendaji kazi.
Aidha, amehimiza kujengwa kwa mazingira ya upendo na ushirikiano mahali pa kazi ili kuongeza ufanisi na mshikamano miongoni mwa watumishi. “Ni wajibu wetu kushirikiana kama familia moja ya Hanang katika kutoa huduma bora kwa wananchi,” alisisitiza.
Watumishi wa mkataba walipata nafasi ya kueleza changamoto zao, huku wengi wakitoa shukrani kwa uongozi wa Halmashauri kwa kuonesha nia ya dhati ya kuwasikiliza na kushughulikia matatizo yao.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: +255 762 362 950
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.