• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Hanang DIstrict Council
Hanang DIstrict Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mpango Mikakati
  • Utawala
    • Organization Structure
    • Idara
      • Utawala na utumishi
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ugavi na Manunuzi
      • Mali Asili
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
    • Viwanda
    • Biashara
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma kwa Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Whe. Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Madiwani
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • On coming Project
    • On going Projects
    • Completed Projects
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shughuli za ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

MKUU WA WILAYA YA HANANG ATOA WITO WA AKIBA YA CHAKULA NA ELIMU AKIFUTURISHA WANANCHI NYUMBANI KWAKE.

Posted on: March 21st, 2025

Katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na Kwaresma, Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Mheshimiwa Almishi Issa Hazali, ameandaa hafla ya futari nyumbani kwake, ikiunganisha waumini wa Kiislamu pamoja na makundi mbalimbali ya jamii.

Tukio hilo limekuwa fursa ya kujenga uhusiano wa kijamii, kuhimiza mshikamano wa kidini na kijamii, na kufikisha ujumbe muhimu wa maendeleo kwa wananchi.

Mheshimiwa Hazali, akizungumza na wageni waalikwa, aliwashukuru wote waliokubali mwaliko huo na kusisitiza umuhimu wa kutunza akiba ya chakula baada ya mavuno. “Hali ya mazao mwaka huu si ya kuridhisha, hivyo ni muhimu kila familia kuhakikisha inaweka akiba ya chakula cha kutosha kabla ya kuuza mazao yote,” alieleza.

Aidha, alihimiza wazazi kuhakikisha watoto wao wanahudhuria masomo kikamilifu, akisema kuwa Serikali imeboresha mazingira ya elimu ili kila mtoto apate nafasi ya kusoma. “Mzazi ana jukumu kubwa la kuhakikisha mtoto wake anapata elimu bora. Serikali imejenga madarasa, imeleta walimu na vifaa vya kujifunzia, hivyo hakuna sababu ya mtoto kubaki nyumbani,” alisisitiza Mkuu wa Wilaya.

Katika hotuba yake, Sheikh wa Wilaya ya Hanang’, Sheikh Muhdi Said Ronka, amepongeza hatua ya Mkuu wa Wilaya kuandaa hafla hiyo, akibainisha kuwa ni kitendo cha kujenga upendo na kusaidiana.

“Kufuturisha ni ibada kubwa yenye malipo makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu. Tunaposhiriki katika matendo haya, tunaimarisha undugu na kuendeleza maadili mema katika jamii,” alisema Sheikh Ronka.

Mmoja wa waumini walioshiriki hafla hiyo, Bi. Amina Juma, alieleza furaha yake kwa tukio hilo, akisema kuwa linasaidia kuimarisha uhusiano kati ya viongozi na wananchi. “Ni jambo jema kuona viongozi wetu wanashiriki nasi katika hafla kama hizi. Inatufanya tujione kuwa sehemu ya jamii yenye mshikamano na amani,” alisema Bi. Amina.

Viongozi wa madhehebu mbalimbali waliokuwepo kwenye hafla hiyo walitumia nafasi hiyo kuwaombea dua viongozi wa wilaya, mkoa na Taifa kwa ujumla, wakisisitiza umuhimu wa kudumisha amani, hususan kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Tukio hilo limeacha athari chanya kwa jamii, likihamasisha umoja na kuhimiza maadili ya kusaidiana katika nyakati muhimu za kiimani.



Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI - HANANG DC October 22, 2024
  • FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA SHULE ZA SEKONDARI WILAYA YA HANANG 2023 December 03, 2022
  • MATOKEO YA USAILI KWA KADA YA MTENDAJI WA KIJIJI III NA KADA YA DREVA II September 12, 2022
  • TANGAZO LA KUKODISHA SHAMBA LA GAWAL NA BASSOTU August 18, 2022
  • View All

Latest News

  • JENGO LA WODI YA WAZAZI HOSPITALI YA TUMAINI MBIONI KUKAMILIKA , LATOA MATUMAINI MAPYA KWA WAKAZI WA HANANG’

    May 14, 2025
  • UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA: WAANDISHI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WAPEWA MAFUNZO HANANG.

    May 14, 2025
  • CCM YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI HANANG’

    May 13, 2025
  • MADIWANI WAPONGEZA UONGOZI KWA HALMASHAURI KWA USIMAMIZI BORA WA MIRADI YA MAENDELEO

    May 07, 2025
  • View All

Video

Mh. Rais John Pombe Maghufuli akitoa onyo juu ya vyombo vya habari
More Videos

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Leseni za Biashara

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi Portal
  • Tovuti yaUtumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali ya Tanzania
  • Tovuti ya Mkoa wa Manyara
  • Tovuti TAMISEMI
  • Mamlaka ya Vitambulisho Tanzania (NIDA)

Watembeleaji wa Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watembelea Tovuti

free HitCounter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward

    Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'

    Telephone: 027-2530022 / 42

    Mobile: +255 762 362 950

    Email: ded@hanangdc.go.tz

Mawasiliano yetu

   

    • Privacy Policy
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.