Afisa Mwandikishaji (RO) wa Jimbo la Hanang, Erick Kayombo, leo Mei 14, amefungua mafunzo ya siku moja kwa Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki ngazi ya Kata kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pilj mzunguko wa pili.
Mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa shule ya msingi Katesh A, yamejikita katika kuwapa mbinu za kitaalamu za kutumia vifaa vya bayometriki na kushughulikia taarifa za wapiga kura kwa usahihi, sambamba na kuzingatia maadili ya kazi na usalama wa vifaa, akiwasisitiza washiriki kutambua uzito wa jukumu walilopewa na kulitendea haki kwa weledi, bidii na uadilifu.
“Kuteuliwa kwenu ni kielelezo cha imani kuwa mna uwezo na uzoefu wa kuhakikisha zoezi hili linafanikiwa kwa viwango vya juu,” alisema Kayombo.
Kayombo amesisitiza kuwa ufanisi wa zoezi hilo unategemea kwa kiasi kikubwa utendaji bora wa kila mshiriki, akionya kuwa uzembe wowote unaweza kuvuruga mchakato mzima. “Kutokuwa makini katika utunzaji wa vifaa kutapelekea athari kubwa katika ukamilishaji wa zoezi hili muhimu,” alionya.
Pamoja na uzoefu walioupata mwaka 2024, washiriki wamehimizwa kutumia maarifa mapya kuhakikisha wananchi wanapata fursa ya kuandikishwa au kusahihisha taarifa zao kwenye daftari la kudumu.
Mafunzo hayo ni sehemu ya maandalizi ya awamu ya pili ya mzunguko wa pili wa uboreshaji wa daftari hilo, chini ya usimamizi wa Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) ambapo kwa wilaya ya Hanang yatafanyika kuanzia Mei 16-25, 2025.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: +255 762 362 950
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.