Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang anawatangazia wakulima na wananchi wote kuwa mauzo ya mazao ya dengu na mbaazi kwa msimu wa mwaka 2025 yatafanyika kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani na minada ya kidijitali (TMX).
Kwa mujibu wa mwongozo wa biashara wa mazao ya dengu, mbaazi, soya, ufuta na choroko wa mwaka 2025, maghala makuu 6 katika kata zifuatazo yatatumika kutekeleza mfumo huu:
1.Gidika (Kata ya Getanuwas)
2.Langwa (Kata ya Nangwa)
3.Endagaw (Kata ya Endagaw)
4.Wareta (Kata ya Wareta)
5.Masqaroda (Kata ya Masqaroda)
6.Boniface Siay (Kata ya Endasak)
Mazao hayo yatakusanywa chini ya usimamizi wa vyama vya wakulima (AMCOS), na hayatakatwa ushuru kupitia mawakala wa kawaida.
⚠️ Onyo: Hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka taratibu rasmi zilizowekwa na serikali.
Mfumo huu unalenga kumwezesha mkulima kupata bei ya ushindani sokoni kwa njia salama na wazi kupitia minada ya kidijitali. Viongozi wa kata na vijiji mnaelekezwa kuendelea kutoa elimu na usaidizi kwa wakulima katika utekelezaji wa mfumo huu.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: +255 762 362 950
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.