Picha mbalimbali zikiwaonyesha Wananchi wa Wilaya ya Hanang' wakiwa kwenye maandalizi ya mwisho kununua mahitaji mbalimbali ya shule kwa ajili ya wanafunzi wao, katika Mnada wa Katesh leo Januari 10, 2026 ikiwa ni maandalizi ya muhula mpya wa masomo unaotarajiwa kuanza Jumanne, Januari 13, 2026.
Ikumbukwe, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang', Teresia Irafay, amewahakikishia wazazi na walezi kuwa maandalizi yote ya kuwapokea wanafunzi wa darasa la awali, darasa la kwanza na wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza yamekamilika.
Akizungumza mwishoni mwa wiki na wakuu wa shule za msingi na sekondari alisema kuwa miundombinu, walimu na mazingira ya shule yapo tayari, na kwamba wanafunzi wote wanapaswa kuanza masomo ifikapo Januari 13, 2026 bila kikwazo chochote.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: +255 762 362 950
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.