Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang', Teresia Irafay, ametoa wito kwa walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari kuimarisha nidhamu ya kuripoti kwa wanafunzi, kuhakikisha kila mtoto anakuwa tayari kuanza masomo Januari 13, 2026.
Katika kikao mahsusi alichongoza leo Januari 8. 226, Irafay amesisitiza umuhimu wa maandalizi ya elimu, akifafanua kwamba wahusika wote wanapaswa kufanya juhudi za kuwakaribisha wanafunzi shuleni.
Irafay pia amewahimiza wazazi na walezi wa watoto waliofaulu mtihani wa kujiunga na kidato cha kwanza kuhakikisha wanafunzi hao wanaripoti shule “hakuna sababu itakayowafanya watoto wasiwasili shuleni,” alisema Irafay, akiongeza kwamba kila mtoto anapaswa kupatiwa nafasi ya kusoma bila vikwazo.
Aidha, amewashauri wazazi kuwasajili watoto ambao wamefikisha umri wa kuanza darasa la kwanza na chekechea, akielezea kuwa walimu wako tayari kuanza masomo mara tu shule zitakapofunguliwa.
Katika taarifa yake, Irafay amethibitisha kuwa miundombinu ya madarasa, madawati, na viwanja vya michezo kwa wanafunzi wakati wakiwa shuleni viko tayari kwa ajili ya wanafunzi wote, ikiwa ni pamoja na wale wenye ulemavu. Hili linadhihirisha dhamira ya Halmashauri ya Wilaya ya Hanang' katika kuhakikisha elimu bora inapatikana kwa watoto wote bila ubaguzi.




Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: +255 762 362 950
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.