Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Hanang' Tarehe 19.02.2024, Limepitisha rasimu ya Mpango na Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Hanang' kwa mwaka 2024/2025.
Baraza hilo lililoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. William Manase. Kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 Jumla ya Shilingi Bilioni 54.2 Halmashauri ya Wilaya ya Hanang' inakadiria kukusanya, kupokea na kutumia.
Akiwasilisha Rasimu hiyo ya Mpango na Bajeti Mkuu wa Divisheni ya Mipango na Uratibu Ndugu Erick Kayombo ambapo pamoja na mambo Mengine amesema:
Halmashauri ya Wilaya ya Hanang' inakadiria kukusanya kupokea na kutumia Jumla ya Shilingi 54,232,827,800.00 kati ya fedha hizo, shilingi 1,451,864,000 sawa na asilimia 2.7 ya Bajeti nzima ni kwaajili ya Matumizi Mengineyo (OC), Shilingi 29,453,952,000.00 sawa na asilimia 54.3 ni kwaajili ya mishahara (PE), Shilingi 15,077,157,000.00 sawa na asilimia 27.8 ni kwaajili ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo na shilingi 8,249,854,800.00 sawa na asilimia 15.2 ya Bajeti nzima ni makusanyo ya ndani ya Halmashauri.
Hata hivo Ndugu Kayombo ameeleza kuwa Bajeti hiyo imezingatia makundi ya msingi yaliyoainishwa kwenye nyaraka muhimu kama vile Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2025, Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Ya CCM ya Mwaka 2020-2025, Sheria ya Bajeti, Mkakati wa Taifa wa Lishe, Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP), Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan wakati analitubia Bunge na Maagizo Mengine Yaliyotolewa na Serikali ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa.
Awali akizungumza wakati wa kikao cha baraza hilo Mhe Manase amesema Rasimu hiyo ya Bajeti ya Kiasi cha Shilingi Bilioni 54.2 itasaidia kuwaletea wananchi maendeleo ikiwa ni pamoja na kuongeza na Kuboresha miundombinu ya huduma za kijamii kama vile Maji, Afya, Mazingira na Miradi mingine Mingi ya Maendeleo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang' Ndugu Francis Namaumbo amesema Bajeti Hii ya Mwaka Wa Fedha 2024/2025 ni lazima itekelezwe kwa kuchukua hatua madhubuti katika ukusanyaji wa mapato ya ndani pamoja na fedha zinazotoka serikali kuu kwaajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo zinasimamiwa vizuri kwa maslahi mapana ya Wananchi na Taifa kwa Ujumla.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: 0787821459
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.