• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Hanang DIstrict Council
Hanang DIstrict Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mpango Mikakati
  • Utawala
    • Organization Structure
    • Idara
      • Utawala na utumishi
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ugavi na Manunuzi
      • Mali Asili
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
    • Viwanda
    • Biashara
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma kwa Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Whe. Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Madiwani
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • On coming Project
    • On going Projects
    • Completed Projects
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shughuli za ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

MILIONI 348.5 KUKAMILISHA UJENZI WA SHULE MPYA YA MSINGI HARARAK

Posted on: May 22nd, 2025

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’ inaendelea kutekeleza kwa vitendo dhamira yake ya kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu nchini, kwa kuwekeza katika miundombinu ya shule katika maeneo yenye uhitaji mkubwa.

Kwa sasa, jitihada hizo zimejikita katika ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi Hararak, iliyopo katika Kata ya Gendabi, Wilaya ya Hanang’. Mradi huu unatekelezwa kwa gharama ya Shilingi milioni 348.5 kwa ufadhili wa Serikali Kuu, na unahusisha ujenzi wa vyumba saba vya madarasa, jengo la utawala, madarasa mawili ya shule ya awali, na vyoo vya kisasa. Ujenzi unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 30 Mei, 2025.

Kwa muda mrefu, watoto kutoka kitongoji cha Hararak walilazimika kutembea umbali mrefu kufuata elimu katika Shule ya Msingi Dumanang, hali iliyosababisha changamoto katika mahudhurio, utoro na uchovu kwa watoto hasa wa darasa la awali. Aidha, ongezeko la wanafunzi katika shule mama ya Dumanang lilizidi uwezo wake wa kawaida.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’, Teresia Irafay, amesema kuwa ujenzi wa shule hii ni sehemu ya mpango mpana wa Serikali wa urejeshaji wa huduma kwa wananchi, hasa katika maeneo yaliyokumbwa na janga la maporomoko ya tope yaliyotokea Desemba 3, 2023.

“Serikali imejizatiti kuhakikisha kuwa kila mtoto anapata elimu katika mazingira salama, rafiki na yanayochochea maendeleo ya kitaaluma. Tunaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi hii ili ifikie malengo yaliyokusudiwa kwa wakati,” amesema Irafay.

Wananchi wa Hararak wameipokea kwa furaha hatua hii ya serikali. Dorika Nantanga, mkazi wa eneo hilo, amesema kuwa ujio wa shule hiyo umerejesha matumaini kwa wazazi na watoto. “Tulikuwa tunahangaika kuwapeleka watoto mbali, lakini sasa huduma iko karibu. Hili ni jambo la kumshukuru Mungu na Serikali,” alisema.

Ujenzi wa shule hii mpya pia unatarajiwa kuongeza uandikishaji wa watoto wa awali na elimu ya msingi, kupunguza utoro, na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa ujumla.

Mradi huu ni miongoni mwa hatua madhubuti zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuhakikisha azma ya “Elimu kwa Wote” inatekelezwa kwa vitendo na kwa usawa katika maeneo yote ya nchi.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI - HANANG DC October 22, 2024
  • FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA SHULE ZA SEKONDARI WILAYA YA HANANG 2023 December 03, 2022
  • MATOKEO YA USAILI KWA KADA YA MTENDAJI WA KIJIJI III NA KADA YA DREVA II September 12, 2022
  • TANGAZO LA KUKODISHA SHAMBA LA GAWAL NA BASSOTU August 18, 2022
  • View All

Latest News

  • HANANG' YAFANYA BONANZA LA USAFI WA MWISHO WA MWEZI

    June 01, 2025
  • MAAFISA ELIMU KATA WAPANGIWA MIKAKATI YA KUINUA UFAULU NA KUDHIBITI UTORO.

    May 31, 2025
  • USAFI NA UTULIVU MJINI: MAMLAKA YA MJI MDOGO KATESH YAJIZATITI KUBORESHA MANDHARI NA USALAMA WA MJI

    May 31, 2025
  • MICHEZO: DED HANANG AWAAGA VIJANA 120 WANAOENDA KUSHIRIKI MASHINDANO YA UMITASHUMTA BABATI

    May 29, 2025
  • View All

Video

Mh. Rais John Pombe Maghufuli akitoa onyo juu ya vyombo vya habari
More Videos

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Leseni za Biashara

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi Portal
  • Tovuti yaUtumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali ya Tanzania
  • Tovuti ya Mkoa wa Manyara
  • Tovuti TAMISEMI
  • Mamlaka ya Vitambulisho Tanzania (NIDA)

Watembeleaji wa Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watembelea Tovuti

free HitCounter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward

    Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'

    Telephone: 027-2530022 / 42

    Mobile: +255 762 362 950

    Email: ded@hanangdc.go.tz

Mawasiliano yetu

   

    • Privacy Policy
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.