Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang wamepata nafasi ya kipekee ya kuonesha umahiri wao katika michezo mbalimbali kupitia bonanza maalumu lililowakutanisha kada tofauti za utumishi wa umma.
Bonanza hilo limefunguliwa rasmi na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Bi. Teresia Irafay, ambaye amewataka watumishi kushiriki kikamilifu kwenye michezo si kwa ajili ya burudani pekee, bali pia kwa kujenga afya, umoja na ushirikiano na kazini.
"Michezo si burudani tu, ni tiba ya mwili na roho. Pia inajenga umoja na upendo miongoni mwa watumishi. Lengo kuu si kushindana kwa nguvu wala kushinda kwa kila namna, bali ni kujenga afya bora, zaidi ya yote, kuleta upendo na umoja kazini" alisema Irafay.
Aidha, alibainisha kuwa bonanza hilo halitakuwa tukio la mara moja bali litafanyika mara kwa mara, kwa lengo la kuimarisha utamaduni wa kupenda michezo na kuongeza ushirikiano wa kijamii.
Washiriki wa bonanza walihusisha watumishi wa kada mbalimbali waliocheza michezo tofauti ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa pete, kuvuta kamba, mbio za mita 100 na michezo ya jadi.
Bonanza hili limeacha tabasamu kubwa kwa washiriki na limeonesha kuwa michezo ni nyenzo muhimu ya kujenga mshikamano kazini na kuimarisha afya za watumishi.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: +255 762 362 950
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.