Halmashauri ya Wilaya ya Hanang imepokea mtambo maalumu wa kuchanganya chumvi na madini muhimu kwa afya, wenye thamani ya shilingi milioni 18, kutoka kwa Ofisi ya Rais (TAMISEMI) kupitia kitengo cha lishe, kwa kushirikiana na Wizara ya Afya.
Mtambo huo utatumika kuchanganya chumvi inayotolewa katika Ziwa la Gendabi kabla ya kusambazwa kwa matumizi ya umma, kuhakikisha ina madini ambayo yana muhimu kubwa kwa kuzuia magonjwa yanayosababishwa na upungufu wa lishe.
Makabidhiano ya mtambo huo yamefanyika mbele ya Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Daniel Luther, ambaye kwa pamoja na Mganga Mkuu wa Wilaya, Dkt. Mohammed Kodi, wameahidi kutumia kifaa hicho kwa lengo lake halisi.
“Tutahakikisha mashine hii inatumika kwa ufanisi kwa maslahi ya wananchi na kuboresha afya ya jamii,” alisisitiza Dkt. Kodi.
Mwakilishi wa TAMISEMI, Hamida Mbilikila, amebainisha kuwa mtambo huo ni sehemu ya mpango wa Rais Samia Suluhu Hassan wa kukabiliana na changamoto za lishe nchini. “Juhudi hizi zinaonesha dhamira ya serikali katika kuhakikisha jamii inakuwa na lishe bora na afya wakati wote” alisema Mbilikila.
Hatua hiyo inatarajiwa kusaidia kuiongezea thamani chumvi inayozalishwa katika Ziwa Gendabi lenye utajiri mkubwa wa madini hayo wilayani Hanang.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: 0787821459
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.