Timu ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang imeendeleza makali yake katika mashindano ya SHIMISEMITA yanayoendelea jijini Tanga, baada ya timu zake zote mbili za Mpira wa Wavu (Volleyball) kuibuka na ushindi wa kishindo.
Upande wa wanawake, Hanang' DC iliichapa Kigamboni MC kwa seti 2-0 (25-21, 25-16), huku wanaume nao wakionyesha moto kwa kuibamiza Karatu DC seti 2-0 (25-6, 25-11). Michezo hiyo ilichezwa jioni ya leo, Agosti 20, 2025, katika viwanja vya Shule ya Sekondari Tanga Tech.
Katika michezo mingine, Hanang' DC imeendelea kufanya vyema kwenye mchezo wa soka (wanaume), na kufikisha alama 9, hivyo kuongoza kundi D2 baada ya kushuka dimbani mara nne.
Mashindano haya yanayoendelea Jijini Tanga, yanapambwa na kaulimbiu isemayo: "Jitokeze Kupiga Kura Kwa Maendeleo Ya Michezo"
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: +255 762 362 950
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.