Halmashauri ya Wilaya ya Hanang imetwaa medali 12 na kombe baada ya kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya SHIMISEMITA 2025 yaliyomalizika jijini Tanga Agosti 29, 2025.
Medali hizo zilitokana na ushindi wa mchezo wa riadha ambapo mshiriki kutoka Hanang', Vicent Kanyogoto alishika nafasi ya kwanza mbio za mita 200 na mita 400, nafasi ya pili katika mbio za mita 100 huku Joseph Ernest akishika nafasi ya nne katika mbio za mita 800 kwa wanaume.
Katika mbio za kupokezana vijiti (relay) kwa wanaume, Hanang' DC ilishika nafasi ya pili kutoka kwa washiriki wake Vicent Kanyogoto, Emanuel Limo, Ally Rajabu na Shafiq Chipembe. Wanawake walishika nafasi ya tatu kutoka kwa washiriki wake Maria Kowero, Aula J. Sheriambaya, Yohana Dominick na Ziada Mwakibango.
Kwa upande wa soka, Hanang' DC ilifika hatua ya nusu fainali, Volleyball wanawake walicheza hatua ya nusu fainali huku wanaume walicheza robo fainali
Kufuatia hatua hiyo kubwa iliyofikiwa, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang' Teresia Irafay ambaye alisafiri na wakuu wa idara kuungana na timu Jijini Tanga kuwatia moyo, aliwapongeza kwa kufanya vizuri katika mashindano hayo na kuahidi kuboresha changamoto zilizojitokeza ili mwakani Hanang' DC ifanye vizuri zaidi.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Hanang', Mwalimu Athumani Likeyekeye alimpongeza Mkurugenzi kwa kuiandaa na kuiwezesha timu yenye ushindani.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: +255 762 362 950
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.