Halmashauri ya Wilaya ya Hanang' imekusudia kutenga maneno kwa ajili ya kuvutia uwekezaji wa ujenzi wa vyuo mbalimbali kikiwemo chuo cha Ualimu na vyuo vya Afya.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang', Teresia Irafay, katika dhifa aliyoiandaa ya kuwakaribisha madiwani wateule, iliyofanyika katika hoteli ya East Side usiku wa Desemba 3, 2025.
Amesema, Halmashauri imekusudia pia kuongeza Zahanati, vituo vya afya kila kata, kuongeza shule za msingi zifike 200 kutoka shule 149 sanjari na kuwa na shule za sekondari zaidi ya 50 kutoka shule karibu 38.
Ili kutekeleza hayo, Irafay ametoa wito kwa waheshimiwa Madiwani wateule wa Halmashauri hii kushikamana na menejimenti ikiwemo kuhamasisha wananchi katika kata zao kuibua na kuanzisha maboma ya miradi mipya ili kupitia fedha za mapato ya ndani zitumike kumalizia maboma hayo.
"Tusipoanzisha wenyewe Serikali inaweza kuleta au isiweze lakini tukiwa na kitu mkononi tunaweza kusapotiwa"
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: +255 762 362 950
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.