Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’ imefanikiwa kuchanja jumla ya mifugo 431,306 tangu kuanza kwa kampeni ya uchanjaji wa mifugo iliyozinduliwa Julai 24, 2025.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Septemba 7, 2025 katika kikao cha tathmini ya zoezi la uchanjaji, idadi hiyo inajumuisha kuku 415,195, ng’ombe 11,426, mbuzi 3,391 na kondoo 1,294. Zoezi hilo linaendelea katika vijiji vyote vya wilaya ya Hanang, likilenga kudhibiti magonjwa na kuboresha afya ya mifugo inayochangia uchumi wa wananchi.
Akizungumza wakati wa kikao hicho kilicholenga kutathmini na kujadili changamoto na mikakati ya kuongeza ufanisi wa kampeni hiyo , Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Teresia Irafay, amewataka wafugaji kutoa ushirikiano wanaposikia ujio wa wataalamu wa mifugo katika maeneo yao
Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Daniel Luther, amebainisha changamoto kadhaa zilizojitokeza katika utekelezaji wa kampeni hiyo, ambazo DED Irafay ameahidi kuzitafutia ufumbuzi wa haraka.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: +255 762 362 950
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.