Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’ imepiga hatua kubwa katika kampeni ya uchanjaji wa mifugo, ambapo hadi kufikia 30 Septemba 2025 jumla ya mifugo 510,729 imekwishapewa chanjo dhidi ya magonjwa mbalimbali, ikilinganishwa na 431,306 iliyokuwa imechanjwa kufikia tarehe 7 Septemba 2025.
Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya Mifugo, ongezeko hilo ni sawa na mifugo 79,423 zaidi, ambalo ni ongezeko la asilimia 18.4% kwa kipindi cha chini ya mwezi mmoja.
Kwa ng’ombe, idadi imeongezeka kutoka 11,426 hadi 62,604 sawa na ongezeko la asilimia 447.8 huku Mbuzi wakiongezeka kutoka 3,391 hadi 18,465 sawa na asilimia 444.6, na kondoo wakiongezeka kutoka 1,294 hadi 8,465, sawa na asilimia 554.0. Aidha, kuku wameongezeka kwa 6,000 pekee, sawa na asilimia 1.4, ikionyesha kuwa kundi hili lilikuwa limefikiwa zaidi mapema katika kampeni.
Mafanikio haya ni ishara ya mwamko mkubwa wa wafugaji kushirikiana na wataalamu wa mifugo, sambamba na mikakati ya halmashauri kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: +255 762 362 950
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.