Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Teresia Irafay, ameipongeza timu ya wanafunzi 120 waliowakilisha Hanang kwenye mashindano ya michezo ya shule za msingi (UMITASHUMTA) kwa kuibuka washindi wa jumla ngazi ya mkoa.
Wilaya ya Hanang imeonesha ubabe wa hali ya juu kwa kutwaa vikombe sita, vikiwemo taji la mshindi wa jumla, katika mashindano yaliyohitimishwa Juni 2, 2025 mjini Babati.
Katika mashindano hayo, timu ya wavulana ya mpira wa miguu iliibuka mabingwa, huku wasichana wakitunukiwa ushindi kwa nidhamu na usafi ulioonekana ndani na nje ya uwanja. Hanang pia ilitawala katika michezo ya goalball, riadha maalum, na soka maalum yote ikiipa wilaya mataji ya ushindi.
Kivutio kingine kikubwa kilikuwa uteuzi wa wanafunzi 26 kutoka Hanang kujiunga na kikosi cha mkoa, kati ya wanafunzi 120 waliokuwa wakishiriki ikiwa ni idadi kubwa zaidi kutoka wilaya moja.
Ufanisi wa Hanang haukuishia kwenye medali pekee. Walimu wanne kutoka wilaya hiyo wameteuliwa kujiunga na benchi la ufundi la timu ya mkoa itakayoiwakilisha Manyara kwenye mashindano ya kitaifa yanayotarajiwa kufanyika mkoani Iringa. Sambamba na hilo, daktari mmoja wa Hanang naye amepewa jukumu la kuungana na timu hiyo kama sehemu ya benchi la kitabibu.
Mashindano ya UMITASHUMTA kwa ngazi ya kitaifa yanatarajiwa kufanyika mkoani Iringa kuanzia Juni 7 hadi 30, 2025.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: +255 762 362 950
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.