Katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika, Katibu Tawala wa Wilaya ya Hanang’, Mwl. Athumani Likeyekeye, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya, Almishi Hazali, ameikumbusha jamii kuendelea kukemea mateso, manyanyaso, mauaji, na vitendo vingine visivyofaa kwa watoto.
Mwl. Likeyekeye ametoa wito huu katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, yaliyofanyika kiwilaya katika ukumbi wa shule ya msingi Katesh A na kuhimiza umuhimu wa kulinda haki za watoto na kuhakikisha wanakuwa katika mazingira salama ya makuzi na kujitambua.
Kwa upande mwingine, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’, Teresia Irafay, amewataka watoto waheshimu wazazi na walezi wao.
Ameongeza kuwa, wakati Serikali, wazazi, na walezi wakijitahidi kutimiza wajibu wao kwao, ni muhimu kwa watoto pia kuwaheshimu wazazi, kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao kwani wao ndilo Taifa la baadae.
Pamoja na mambo mengine, maadhimisho haya yamefanyika kwa kufanya maandamano ya amani ambapo, Mkurugenzi wa Halmashauri, Teresia Irafay amewatembeza watoto hao katika Stendi mpya ya mabasi Katesh, ili waweze kujionea uwekezaji ambao Serikali imefanya.
Siku ya Mtoto wa Afrika huadhimishwa kila mwaka tarehe 16 Juni ili kukumbuka na kusherehekea haki za watoto barani Afrika. Maadhimisho haya yanatokana na matukio ya kihistoria yaliyotokea mwaka 1976 katika jiji la Soweto, Afrika Kusini.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: +255 762 362 950
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.