Timu ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang', leo Septemba 8, 2025 imewasilisha medali 12 na kombe kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang', Teresia Irafay, zilizotokana na kufanya vizuri katika mashindano ya Shirikisho la Michezo Serikali za Mitaa (SHIMISEMITA) yaliyofanyika Jijini Tanga.
Medali hizo za ushindi zimekabidhiwa na Mkuu wa Idara ya Utumishi na Rasilimali Watu, Lucy Kaulule mbele ya wakuu wa idara mbalimbali na baadhi ya wanamichezo walioshiriki mashindano hayo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo fupi, Irafay amewapongeza wanamichezo wote waliojitoa kuhakikisha ushindi huo unapatikana na kusisitiza umuhimu wa maandalizi ya mapema kwa kuandaa mabonanza ya michezo ambayo yatawaweka tayari muda wote ili mwakani Hanang' ikafanye vizuri zaidi.
Aidha, amesema ataendelea kutenga fedha kutoka mapato ya ndani ili kuboresha viwanja vya michezo.
Mkuu wa msafara katika mashindano ya SHIMISEMITA, Justine Martin, ambaye pia ni Afisa Utumishi ametoa shukrani kwa Mkurugenzi kwa juhudi zake zilizochochea mafanikio hayo, huku Afisa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bernard Sambagi, akieleza kuwa kuelekea mashindano hayo mwakani, maandalizi yataanza mapema na kusema kuwa ushindi huo ni matokeo ya jitihada za pamoja, viongozi na washiriki.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: +255 762 362 950
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.