Muu wa Wilaya ya Hanang, Mheshimiwa Almishi Hazali, leo Julai 22, 2025 amefungua rasmi Ligi ya Soka ya Wilaya ya Hanang katika hafla iliyofanyika katika Uwanja wa Mount Hanang, mojawapo ya miradi iliyotembelewa na Mwenge wa Uhuru 2025.
Ligi hiyo inajumuisha jumla ya vilabu 21 kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Hanang, ikiwa ni jukwaa mahsusi kwa vijana kuonesha vipaji vyao na kukuza mshikamano wa kijamii kupitia michezo.
Katika kuonesha dhamira ya kuendeleza michezo, Mheshimiwa Hazali alikabidhi mchango wa shilingi 1,000,000 kusaidia uendeshaji wa ligi hiyo, fedha ambazo zitatumika katika kugharamia mahitaji mbalimbali kama waamuzi, vifaa vya michezo, na ustawi wa wachezaji.
“Ligi hii si tu mashindano ya mpira wa miguu, bali ni sehemu ya kujenga umoja, kukuza vipaji, na kutoa fursa kwa vijana wetu kung’ara kitaifa,” alisema DC Hazali wakati wa hotuba yake ya uzinduzi.
Mashabiki wa soka kutoka maeneo mbalimbali walijitokeza kwa wingi kuushuhudia mchezo wa ufunguzi, huku uwanja ukilipuka kwa vifijo, nderemo na rangi za vilabu pinzani.
Ligi ya Wilaya ya Hanang inatarajiwa kudumu kwa kipindi cha wiki kadhaa, ikifanyika katika uwanja wa Mount Hanang Stadium.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: +255 762 362 950
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.