Wilaya ya Hanang ni miongoni mwa Wilaya tano zinazounda Mkoa wa Manyara. Wilayahii ni miongoni mwa Wilaya za Tanzania zilizoadhimisha sherehe za miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka 2024.
Kushiriki zoezi la Usafi
Katika tukio hili Mhe. Mkuu wa Wilaya tarehe 24/04/2024 akiwa na viongozi wengine wa Wilaya, wakuu wa Idara pamoja na vitengo vya Halmashauri waliungana na wananchi kushiriki zoezi la kufanya usafi katika soko la Katesh. Pamoja na zoezi a usafi, Mhe. Mkuu wa Wilaya aliwahutubia wananchi juu ya masuala mbalimbali yanayohusu umuhimu na faida za Muubgano.
Zoezi la upandaji miti
Wilaya ya Hanang iliungana na wananchi na viongozi mbalimbali kupanda miti katika kuadhimisha Muungano. Jumla ya miti 300ya aina mbalimbali ilipandwa katika eneo la shule ya Sekondari Lalaji. Zoezi hili lilisimamiwa na Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Hanang kwa kushirikiana na TFS pamoja na wadau mbalimbali
Aidha wanafunzi wa shule ya Sekondari Lalaji pamoja na kupanda miti walishiriki katika kuimba nyimbo mbalmbali zinazohusiana na Muungano wa Tanzania na Zanzibar. Pia wazee wa mila na viongozi wa dini waliokuwa wamealikwa walipewa nafasi ya kuliombea Taifa na kuuombea Muungano wa Tanzania.
Ufuatiliaji wa Hotuba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Katika usiku wa kuamkia tarehe 26 Aprili, 2024 wananchi katika maeneo mbalimbali yakiwemo Balangdalalu, Katesh na Bassotu walifuatilia Hotuba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusiana na Muungano wa Tanzania.
Hotuba kwa wananchi
Mhe. Mkuu wa Wilaya alihutubia wananchi wa kata ya Lalaji na maeneo ya jirani waliokuwa wamekusanyika katika viwanja vya sekondari ya Lalaji. Katika hotuba hiyo Mkuu wa Wilaya alipongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna navyoendeleza na kuenzi Muungano. Aidha aliwahimiza wananchi kullnda na kuuenzi Muungano kwa manufaa ya sasa na ya baadaye.
Hitimisho
Sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimefanyika na kuhitimishwa katika maeneo mbalimbali ya Wilaya. Aidha wananchi wameelimishwa na kuelewa juu ya dhana nzima ya Muungano. Wilaya itaendelea kuelimisha wananchi juu ya jambo hili ili kuendelea kujenga uzalendo na uelewa wa pamoja kwa vizazi vyote.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: 0787821459
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.