Wananchi Wilaya Hanang Mkoani Manyara wameshauriwa kuitumia elimu ya sheria waliyoipata katika maadhimisho ya wiki ya sheria nchini kutatua changamoto zinazowakabili, badala ya kujichukulia sheria mkononi.
Rai hiyo ilitolewa na Katibu Tawala Wilaya ya Hanang, Athumani Likeyekeye, alipomwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Almishi Hazali katika Kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria nchini kiwilaya yaliyofanyika katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya.
"Hii wiki imetumika vizuri na sisi Wanahanang tunapongeza sana Mahakama yetu Tanzani lakini kupitia Mahakama yetu ya wilaya, kazi mliyoifanya ni kubwa. Haki inapotendeka hata sisi katika kusimamia maendeleo ya Taifa letu linakuwa ni jambo jepesi, hongereni sana na Mungu atawabariki" alisema Likeyekeye
Kwa upande wake, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Hanang, Mheshimiwa Arnold Kileo alisema katika kutekeleza mpango wa Taifa wa mwaka 2050, Mahakama inajukumu la kuhakikisha sheria zinatekelezwa kwa ufanisi ili kusaidia kuimarisha utawala wa sheria kwa kuhakikisha haki inapatikana kwa wote.
Kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria nchini chenye kaulimbiu isemayo "Tanzania ya 2050: Nafasi ya Taasisi zinazosimamia haki madai katika kufikia malengo makuu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo", kilichofanyika Februari 3, 2025 ambapo kitaifa maadhimisho yamefanyika mkoani Dodoma na mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: 0787821459
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.