Watumishi wa Umma halmashauri ya Wilaya ya Hanang, wameshauriwa kutumia maarifa na ujuzi walionao kutatua changamoto za wananchi kila mtu kulingana na nafasi yake katika utumishi.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Teresia Irafay, wakati akihitimisha mafunzo maalum kwa watumishi wapya walioajiriwa, wakiwemo kada ya afya, mifugo, na utawala, kikao kilichofanyika leo Februari 20, 2025 katika ukumbi wa hospitali ya Wilaya, Tumaini.
Amewakumbusha watumishi kumtanguliza Mungu katika kila jambo kabla ya kufanya uamuzi ili uamuzi huo uwe wa manufaa kwa jamii wanayoiongoza na kwao, kujiepusha kutumia fedha za michango ya wananchi bila utaratibu na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya serikali.
Aidha, amewakumbusha kuwa wabunifu katika kazi, kuwaheshimu viongozi, kujishughulisha katika shughuli za kijamii ikiwemo misiba na sherehe, kuzingatia mavazi yenye stara sanjari na kujiepusha na kashfa zinazoweza kupelekea wakose sifa za utumishi wa Umma.
Pia amewahamasisha watumishi kujihusisha na michezo kwa kile alichodai inaimarisha afya huku akiwakumbusha kujiendeleza kielimu ili waweze kujiweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya utumishi.
Kwa upande wao baadhi ya watumishi waliopata nasaha hizo wamempongeza Mkurugenzi Mtendaji kwa namna alivyowakumbusha wajibu wao na kuahidi kwenda kuyatekeleza ili wananchi wapate huduma bora.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: 0787821459
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.