MKUTANO WA KAWAIDA WA BARAZA LA MADIWANI KUJADILI TAARIFA ZA HALMASHAURI ROBO YA TATU (JANUARI – MACHI) 2016/2017.
Mkutano wa tatu wa kawaida wa Baraza la Madiwani kwa mwaka 2016/2017 kilifanyika jana katika ukumbi mkuu wa Halmashauri Tarehe 28/04/2017. Mkutano huo umeudhuriwa na wajumbe wa Baraza akiwemo Mbunge wa Jimbo Hanang’ Mhe. Dr.Mary Michael Nagu, Waheshimiwa Madiwani, Wakuu wa Idara/Vitengo pamoja na Viongozi mbalimbali waalikwa. Mkutano huo ulifunguliwa na Mwenyekiti wa Mkutano wa Baraza Mhe. George G. Bajuta asubuhi saa 4:00am na kumalizika majira ya jioni saa 12:10pm.
Lengo kuu la Mkutano
Mkutano wa Baraza la Madiwani kilikaa kwa mujibu wa sheria kwa lengo la kujadili taarifa za Halmashauri kwa robo ya tatu Januari –Machi kwa mwaka 2016.2017 pamoja na kuweka maazimio mapya kwaajili ya maendeleo na ustawi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’.
Mambo muhimu yaliyozungumzwa na Viongozi mbalimbali katika Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Tarehe 28/04/2017
Mkuu wa Wilaya Hanang’
Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya, Ndg. Sara Sanga ambaye pia ni Katibu Tawala Wilaya Hanang, kupitia Mkutano huo wa BarazalaMadiwani aliwahasa wananchi wa Hanang’ kuhifadhi chakula na kuachana na tabia ya kuuza mazao yao ya chakula wanayovuna hivi sasa hususani maharagwe kwani hali ya chakula Wilayani hapa sii nzuri. Aidha aliwashauri wafugaji kuuza baadhi ya mifugo yao ili kuweza kununua mazao ya chakula kuepukana janga la njaa.
Mbunge wa Jimbo Hanang’
Mkutano huo wa Baraza la Madiwani pia ulihudhuriwa Mbunge wa Jimbo la Hanang’ Mhe. Dr.Mary Michael Nagu ambapo aliipongeza Halmashauri kwa kutambua umuhimu wa kuzipongeza shule 10 bora zilizofanya viruzi katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba kwa mwaka 2016 Wilayani Hanang’. Aidha aliwaasa wadau wote wa Elimu kushirikiana kwa pamoja kwa lengo la kuinua Elimu wilayani Hanang, sambamba na hilo aliwaomba viongozi wote kuondoa itikadi zao za vyama na kushikamana kwa lengo la kujenga maendeleo ya Halmashauri ya Wilaya ya Hanang.
Mkutano wa Baraza kuwapongeza shule zilizofanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya darasala Saba Hanang’ 2016.
Katika mkutano huo wa tatu wa Baraza la Madiwani, iliwatunuku zawadi shule 10 bora za Hanang zilizofanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2016.
Zawadi mbali mbali zilitolewa kwa Walimu Wakuu wa shule hizo pamoja na Maafisa Elimu Kata wa maeneo ya shule hizo. Zawadi zilizotolewa ni pamoja na fedha Taslimu, vyeti na barua za pongezi.
Lengo la kutolewa kwa zawadi hizo ni moja ya mikakati ya Halmashauri kuinua kiwango cha Elimu Wilayani Hanang’ kwa kutoa Motisha kwa shule zitakazokuwa zikifanya vizuri na hivyo kutia chachu kwa shule zingine kuweza kufanya vizuri.
Shule 10 bora zilizopongezwa na kutolewa zawadi;
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: 0787821459
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.