Mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’ umefanyika leo Desemba 3, 2025 katika ukumbi wa Halmashauri, ambapo madiwani wateule wameapishwa rasmi na kuanza kutekeleza majukumu yao ya kiuongozi.
Katika mkutano huo, Diwani wa Kata ya Simbay, Mheshimiwa George Bajuta, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’, huku Diwani wa Kata ya Dawar, Charles Yona, akichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti.
Katika Hotuba yake, Mhe. Bajuta ameahidi ushirikiano, uwazi na uwajibikaji katika kuongoza baraza hilo katika kipindi cha miaka mitano ijayo huku akitaja vipaumbele kuwa ni pamoja na kuongeza mapato kutoka bilioni 6 hadi bilioni 10 ili fedha zitakazopatikana zikatekeleze miradi ya maendeleo na ameahidi kuboresha miundombinu kwa kununua mitambo ya kuchonga barabara.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: +255 762 362 950
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.