Tarehe Mosi Aprili ya kila mwaka ni siku ya maadhimisho ya siku ya upandaji Miti Ki-taifa. Siku hii hutumika kuhamasisha wananchi kutekeleza agizo muhimu la Ki-taifa la kupanda Miti ili kukabiliana na kasi kubwa ya uharibifu wa Misitu Nchini.
Misitu hii zinaangamizwa kila mwaka kutokana na sababu mbalimbali ikiwepo:-
Ili kurejesha Misitu Nchini, kiasi cha hekta 185,000 zinatakiwa kupandwa Miti kila mwaka kwa mfululizo kwa miaka 17.
Serikali imeweka mikakati mbalimbali ya kukabiliana na hali hii ambayo ni :-
Maadhimisho ya siku ya upandaji miti Wilaya ya hanang’
Katika kutekeleza agizo la Serikali,Wilaya ya Hanang’ imeweka mikakati na malengo ya kupanda Miti 1,500,000 kila mwaka kama ifuatavo:-
Leo katika maadhimisho haya Halmashauri ya Wilaya ya Hanang' imepanda jumla ya Miti 1600 ya aina mbalimbali sawa na eneo la hekta moja kwenye maeneo yanayozunguka Ofisi za Halmashauri, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na eneo la hifadhi ya Mlima Ganana, lengo kuu likiwa ni kuhifadhi Mazingira yanayozunguka Ofisi zote, pia kuhifadhi eneo la Mlima Hanang’
Katika kuadhimisha siku hii, Viongozi mbalimbali wa Wilaya, Jeshi la Polisi, Watumishi pamoja na Wananchi, walishiriki katika zoezi la upandaji miti katika maeneo mbalimbali.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: 0787821459
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.