Mwenge wa Uhuru 2025 umepokelewa rasmi leo Julai 12 , 2025 mkoani Manyara ukitokea mkoani Arusha, katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Mererani wilayani Simanjiro.
Akizungumza baada ya kupokea Mwenge huo, Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mheshimiwa Queen Sendiga amesema Mwenge wa Uhuru utapita katika wilaya zote za mkoa, ambapo utatembelea, utakagua na kuzindua miradi 51 yenye thamani ya shilingi bilioni 71.3.
Mheshimiwa Sendiga amesisitiza kuwa miradi hiyo inagusa sekta muhimu kama maji, afya, elimu, miundombinu na uwezeshaji wa wananchi kiuchumi, ikiwa ni ishara ya dhamira ya serikali kuboresha maisha ya wananchi wa Manyara.
Kwa Wilaya ya Hanang, Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kupokelewa Julai 18, 2025 katika viwanja vya shule ya msingi Dabaschand. Aidha, mkesha wa Mwenge umepangwa kufanyika katika stendi ya zamani mjini Katesh, ambapo wananchi wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki.
Wilaya ya Hanang imeshiriki mapokezi ya Mwenge wa Uhuru leo Mererani kwa uongozi wa Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Almishi Hazali, akiongozana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang Teresia Irafay, Katibu Tawala Wilaya Mwl. Athumani Likeyekeye na Mratibu wa Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Hanang, Bernard Sambagi.
Viongozi hao wamesema wilaya imejipanga vizuri kupokea Mwenge kwa kuhakikisha usalama, maandalizi ya miradi itakayotembelewa, pamoja na kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kudumisha amani na mshikamano.
Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2025 inawahimiza wananchi: “Jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu kwa amani na utulivu.”
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: +255 762 362 950
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.