• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Hanang DIstrict Council
Hanang DIstrict Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mpango Mikakati
  • Utawala
    • Organization Structure
    • Idara
      • Utawala na utumishi
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ugavi na Manunuzi
      • Mali Asili
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
    • Viwanda
    • Biashara
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma kwa Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Whe. Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Madiwani
      • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Ukimwi
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • On coming Project
    • On going Projects
    • Completed Projects
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shughuli za ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

PAC YAPONGEZA UJENZI NYUMBA 109 KWA WAATHIRIKA WA MAPOROMOKO YA TOPE HANANG.

Posted on: March 17th, 2025

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imepongeza Serikali kwa ujenzi wa nyumba 109 kwa waathirika wa maporomoko ya tope yaliyotokea Desemba 2023 mkoani Manyara.

Kamati imetoa pongezi hizo tarehe 17 Machi, 2025 wakati wa ziara yao katika kitongoji cha Waret kilichopo wilayani Hanang Mkoani Manyara kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa nyumba 109 kwa waathirika pamoja na ujenzi wa shule mpya ya msingi iliyojengwa katika kitongoji hicho.

Akizungumza mara Baada ya ukaguzi wa eneo hilo , Mwenyekiti wa kamati hiyo na Mbunge wa Vwawa, Mhe. Japhet Hasunga, amesema wameridhishwa na utekelezaji wa miradi iliyopo pamoja na thamani ya fedha iliyotumika unaakisi ubora wa kazi.

"Kwanza tunampongeza Daktari Samia Suluhu Hassan ambaye aliona hili pamoja na viongozi wengine wote waliosimamia mradi huu, tumeona fedha za umma zikitumika kwa ufanisi, na hii ni ishara nzuri ya usimamizi mzuri wa miradi ya kimaendeleo hivyo tuhakikishe tunailinda na kuendeleza kwa ubora unaohitajika ," alisema Mhe. Hasunga,

Katika taarifa yake, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amesema, ujenzi wa nyumba hizo ni sehemu ya mkakati wa serikali wa kurejesha hali ya kawaida kwa waathirika wa maporomoko hayo.

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akitoa taarifa ya ujenzi wa Nyumba 109 mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya PAC.

(Picha na: Mwalimu Carol Gisimoy)

Pamoja na ujenzi wa nyumba, serikali imekamilisha ujenzi wa shule mpya ya msingi katika eneo hilo, yenye thamani ya zaidi ya shilingi ya milioni 490, ambayo mpaka sasa inahudumia zaidi ya wanafunzi 600, ikiwa na madarasa ya kisasa, ofisi za walimu pamoja na vyoo.

"Nyumba hizi zimejengwa katika eneo la Waret Kijiji cha Gidagamond, Kata ya Mogitu, Wilaya ya Hanang , Eneo zilipojengwa nyumba hizo lilikuwa linamilikiwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jeshi la Magereza na sasa eneo hilo linamilikiwa na Halmshauri ya Wilaya ya Hanang’”

“Aidha, ujenzi wa nyumba umefanyika katika viwanja 109 vya ukubwa wa mita za mraba 800 kwa kila kiwanja kati ya viwanja 226 katika Kitalu A. Kila n TC nyumba ina ukubwa wa mita za mraba 29 ikijumuisha vyumba vitatu vya kulala, sebule, baraza, jiko la nje, bafu na choo cha nje. Ujenzi ulisimamiwa na Timu ya Wataalam kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu); Ofisi ya Rais – TAMISEMI; Wizara ya Fedha; Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara; na Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’”. aliongeza Dkt. Yonaz.

Katika hatua nyingine, Dkt. Yonaz amebainisha kuwa, serikali ipo katika mchakato wa kufunga vifaa maalum vya ufuatiliaji wa mwenendo wa Mlima Hanang ili kutoa tahadhari za mapema endapo kutatokea hali isiyo ya kawaida kama maporomoko au mafuriko.

"Tumejifunza kutokana na janga hili, na sasa tunachukua hatua za kisayansi kuhakikisha tunazuia madhara makubwa siku zijazo," alisema Dkt. Yonaz.

TAZAMA VIDEO HAPA

Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeongeza matumaini kwa wananchi wa Hanang, ambao sasa wanashuhudia juhudi za serikali katika kuhakikisha ustawi wao unaboreshwa ambapo Serikali imesisitiza kuwa itaendelea kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha inawanufaisha wananchi kwa ufanisi na uwazi.



Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI - HANANG DC October 22, 2024
  • FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA SHULE ZA SEKONDARI WILAYA YA HANANG 2023 December 03, 2022
  • MATOKEO YA USAILI KWA KADA YA MTENDAJI WA KIJIJI III NA KADA YA DREVA II September 12, 2022
  • TANGAZO LA KUKODISHA SHAMBA LA GAWAL NA BASSOTU August 18, 2022
  • View All

Latest News

  • UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA: WAANDISHI WASAIDIZI NA WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WAPEWA MAFUNZO HANANG.

    May 14, 2025
  • CCM YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI HANANG’

    May 13, 2025
  • MADIWANI WAPONGEZA UONGOZI KWA HALMASHAURI KWA USIMAMIZI BORA WA MIRADI YA MAENDELEO

    May 07, 2025
  • ZAIDI YA BILIONI 1.3 ZAKOPESHWA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU, SERIKALI YASISITIZA UWAJIBIKAJI.

    May 03, 2025
  • View All

Video

Mh. Rais John Pombe Maghufuli akitoa onyo juu ya vyombo vya habari
More Videos

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu za Leseni za Biashara

Viunganishi Linganifu

  • Watumishi Portal
  • Tovuti yaUtumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali ya Tanzania
  • Tovuti ya Mkoa wa Manyara
  • Tovuti TAMISEMI
  • Mamlaka ya Vitambulisho Tanzania (NIDA)

Watembeleaji wa Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watembelea Tovuti

free HitCounter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward

    Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'

    Telephone: 027-2530022 / 42

    Mobile: +255 762 362 950

    Email: ded@hanangdc.go.tz

Mawasiliano yetu

   

    • Privacy Policy
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.