Kamati ya Afya ya Msingi ya Wilaya ya Hanang' imefanya kikao muhimu tarehe 7 Januari 2026, chini ya uenyekiti wa Mheshimiwa Almishi Hazali, Mkuu wa Wilaya ya Hanang', kilicholenga kuwajengea uwezo wakuu wa idara na vitengo kuhusu mkakati wa uhamasishaji wa Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote.
DED Irafay amesema hayo katika kikao cha kuwajengea uwezo wakuu wa idara na vitengo kuhusu mkakati wa uhamasishaji wa Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote. kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri, ni miongoni mwa ahadi kuu za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyeahidi kuanza utekelezaji wa mpango huo ndani ya siku 100 za kwanza baada ya kuapishwa.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Hanang Mheshimiwa Almishi Hazali amesisitiza umuhimu wa viongozi na wataalamu wa afya kushirikiana kwa karibu kuhakikisha wananchi wanaelimishwa ipasavyo kuhusu faida za bima ya afya, akibainisha kuwa mpango huo utasaidia kupunguza gharama za matibabu na kuongeza upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi wote.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Teresia Irafay, amesema kuwa ofisi yake kwa kushirikiana na wataalamu wa sekta ya afya imejipanga kikamilifu kuhakikisha elimu kuhusu bima ya afya kwa wote inawafikia wananchi kwa haraka na kwa usahihi, kupitia mikutano ya hadhara, vituo vya afya na ngazi za jamii.
Amesema uelewa sahihi wa wananchi kuhusu mpango huo ni msingi wa mafanikio yake, huku Halmashauri ikiendelea kuweka mazingira wezeshi ili kuhakikisha kila mwananchi anapata fursa ya kunufaika na huduma za afya bila vikwazo vya kifedha.





Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: +255 762 362 950
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.