Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mheshimiwa Almishi Hazali amesema serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika jitihada za kuboresha sekta ya kilimo wilayani Hanang ili kuwasaidia wakulima kupata ushauri wa kitaalamu, mbegu bora, na viuatilifu, hatua inayochangia ongezeko la uzalishaji wa mazao.
Mhe. Hazali ameyasema hayo leo alipokuwa akitembelea mashamba ya wakulima katika kijiji cha Dawar, ambapo alishuhudia maendeleo yanayopatikana kupitia msaada wa wadau mbalimbali wa kilimo katika hafla maalumu iliyoandaliwa na idara ya kilimo na Uvuvi ya halmashauri ya wilaya Hanang.
Mkuu wa Wilaya, Mhe. Almishi Hazali, ameishukuru sekta binafsi kwa kushirikiana na serikali kupitia Idara ya Kilimo na Uvuvi kwa kuendelea kutoa ushirikiano muhimu na wataalamu wa kilimo kutoka halmashauri na kuhakikisha huduma za ugani zinawafikia wakulima kwa wakati sahihi.
Hafla hiyo imewakutanisha wadau wa sekta ya kilimo, wakiwemo wazalishaji wa mbegu bora za mahindi, alizeti, na maharage, pamoja na wakulima wa eneo hilo, wakijadili namna bora ya kuongeza tija.
Akizungumza katika tukio hilo, Mkuu wa Idara ya Kilimo na Uvuvi wa Wilaya ya Hanang, Daniel Luther, amesema mpango huo unalenga kuboresha huduma za ugani kwa kuwafikia wakulima moja kwa moja mashambani, kusikiliza changamoto zao, na kutafuta suluhisho kwa kushirikiana na wataalamu wa kilimo.
Luther amepongeza wadau wa kilimo kwa juhudi zao za kuleta maendeleo katika wilaya hiyo na kusisitiza kuwa serikali itaendelea kushirikiana nao kuhakikisha wakulima wanapata mbinu za kisasa za kilimo.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, John Kajivo amesema serikali inaendelea kushirikiana na sekta binafsi ili kuhakikisha kila kijiji kinapata huduma za wataalamu wa kilimo, jambo linalolenga kuongeza uzalishaji na kuboresha maisha ya wakulima.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: 0787821459
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.