Serikali Wilaya ya Hanang, imesema itakumbuka na kuenzi mchango wa marehemu, Padri Magnus Lochbihler alioutoa katika jamii enzi za uhai wake, hususani katika sekta ya elimu, utunzaji wa mazingira na huduma ya kiroho.
Akitoa salamu za Serikali za pole kwa waumini wa Kanisa Katoriki, Jimbo la Katoliki la Mbulu, Parokia ya Mtakatifu Mathias, Afisa Tawala wa Wilaya ya Hanang Hamad Kaaya aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Mheshimiwa Almishi Hazali, amesema, Padri Magnus Lochbihler enzi za uhai wake alijenga hosteli jirani na shule ya sekondari Gitting na alikuwa mdau wa mazingira baada ya kuanzisha upandaji miti katika viunga vya kanisa Katoliki Parokia ya Gitting.
"Ile hosteli imekuwa msaada mkubwa sana kwa wanafunzi wanaotoka mbali wamekuwa wakikaa pale na wameweza kupata elimu"
Aidha, amesema Serikali itaenzi mchango huo kwa kuendelea kuhamasisha jamii kupanda miti pamoja na kujitolea katika mambo ya kijamii.
Katika mazishi hayo, walihudhuria pia viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang.
Marehemu, Padri Magnus Lochbihler alifariki Februari 13, 2025 na kuzikwa Februari 20, 2025 katika viunga vya Kanisa Katoliki, Parokia ya Gitting akiwa na umri wa miaka 95.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: 0787821459
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.