Timu ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang imeendelea kuwa moto wa kuotea mbali katika mashindano ya SHIMISEMITA yanayoendelea jijini Tanga baada ya kutinga hatua ya nusu fainali kupitia michezo ya soka na volleyball.
Katika mchezo wa mapema jana asubuhi, wanawake wa Hanang DC walionesha ubabe mkubwa kwenye mchezo wa volleyball kwa kuichapa Karatu DC seti 3–0 (25–20, 25–17, 25–12) na kufuzu hatua ya nusu fainali kwa kishindo.
Baadaye jioni, mchezo wa soka uliweka historia yake, baada ya wanaume wa Hanang DC kutinga nusu fainali kwa mikwaju ya penalti 3–2 dhidi ya Pangani DC, kufuatia dakika 90 za mchezo kumalizika kwa sare tasa bila kufungana.
Kilichoongeza msisimko wa michezo yote ni uwepo wa viongozi wakuu wa wilaya hiyo, akiwemo Katibu Tawala wa Wilaya ya Hanang, Mwl. Athumani Likeyekeye, na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Teresia Irafay, waliokuwa bega kwa bega na wakuu wa idara mbalimbali kuiunga mkono timu yao.
Ikumbukwe, Hanang DC tayari imejihakikishia heshima katika michezo ya riadha baada ya kutwaa medali kwenye mbio za mita 100, 200, 400 pamoja na mbio za kupokezana vijiti (relay) kwa wanaume na wanawake.
Kwa hali hii, Hanang DC sasa imebaki kuwa miongoni mwa halmashauri tishio zaidi kwenye mashindano ya SHIMISEMITA 2025.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: +255 762 362 950
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.