Wanariadha wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’ wameandika historia mpya baada ya kutwaa medali katika mbio za kupokezana vijiti (relay) kwenye mashindano ya SHIMISEMITA yanayoendelea jijini Tanga.
Katika michezo ya riadha kwa wanaume, Hanang’ DC imeendelea kung’ara baada ya kufuzu hatua ya nusu fainali katika mbio za mita 100, mita 400 na mbio za kupokezana vijiti (Relay - mita 400), ikiweka matumaini ya ushindi zaidi kuelekea hatua za mwisho.
Hatua hii inakuja sambamba na mafanikio ya timu hiyo katika michezo mingine, ambapo Hanang’ DC tayari imesonga mbele kwenye volleyball na soka, na kuendelea kuonesha ubora na uimara wa kikosi chake katika michezo tofauti.
Kwa ujumla, kasi na morali ya wachezaji wa Hanang’ DC inaifanya timu hiyo kuendelea kuwa kivutio kikuu kwenye mashindano haya, huku matarajio ya kutwaa mataji zaidi yakiendelea kushika kasi.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: +255 762 362 950
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.