Wilaya ya Hanang imeadhimisha siku ya mazingira Duniani katika kata ya Ganana eneo la soko kuu ambapo mh mkuu wa wilaya Miss Sara Msafiri alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na mamia ya wananchi wa Wilaya ya Hanang.
Mamia ya Wananchi wa Hanang waliohudhuria maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani wakipata elimu juu ya matumizi ya Nishati mbadala
Mh Mgeni Rasmi Mhe mkuu wa wilaya ya hanang Sara Msafiri katika hotuba yake amewaasa wananchi wa Hanang kuhakikisha wanautunza mlima Hanang kwani ndio chanzo kikuu cha maji na maji ndio changamoto kubwa kwa wananchi wa Hanang.Aidha mkuu huyo wa wilaya amewataka wananchi kutumia nishati mbadala ili kupunguza matumizi ya mkaa wa miti ambao ndio chanzo kikuu cha uharibifu wa mazingira
mkuu wa wilaya akikagua nishati mbadala ya mkaa wa karatasi iliyotengenezwa na kikundi cha Sayuni.
Aidha mkuu wa wilaya amewatunuku vyeti na zawadi mbalimbali wadau wa mazingira wilayani hanang.Baadhi ya waliopatiwa tunu hizo ni pamoja na Diwani wa Gidahababieg Mhe Hassan Hilbagiroy aka Mzee wa Dawa mwingine ni Mwenyekiti wa soko kuu.
Mwenyekiti wa soko kuu akipokea cheti cha pongezi kwa niaba ya wanasoko wote
Mhe Hssan Hilbagiroy akipokea cheti cha Pongezi
Mwakilishi wa kampuni ya mobisol akipokea cheti cha pongezi kwa kuwa wadau wa mazingira kwa kusambaza nishati mbadala wilaya ya hanang.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: 0787821459
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.