Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Maryam Muhaji, ameongoza kikao kazi cha uwasilishaji wa mpango wa gharama za utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Maji na Usafi wa Mazingira (WASH) kilichofanyika Novemba 13, 2025, katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang.
Akizungumza wakati wa kikao hicho, Muhaji amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wadau wote wa sekta ya maji, afya, elimu na jamii kwa ujumla katika utekelezaji wa programu hiyo, akibainisha kuwa lengo kuu ni kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma bora, endelevu na salama za maji na usafi wa mazingira.
Amesema kuwa serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo inaendelea kuweka mikakati madhubuti ya kuboresha huduma za maji vijijini na mijini, ili kufikia malengo ya kitaifa ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa kila kaya ifikapo mwaka 2030.

Aidha, Muhaji amewataka washiriki wa kikao hicho kuhakikisha mipango na bajeti zitakazowasilishwa zinaendana na vipaumbele vya wananchi, huku akisisitiza umuhimu wa uwajibikaji, ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa ufanisi zaidi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang Teresia Irafay, pamoja na wataalamu kutoka sekta mbalimbali, wamewasilisha taarifa na mikakati ya utekelezaji wa programu hiyo katika ngazi ya wilaya, wakiahidi kuendelea kushirikiana kwa karibu na serikali ya mkoa na wadau wote husika.
Kikao kazi hicho kimehudhuriwa na wataalamu kutoka ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa, viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, wawakilishi wa taasisi za serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, pamoja na wadau wa maendeleo wanaoshiriki katika sekta ya maji na usafi wa mazingira.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: +255 762 362 950
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.