Katibu Tawala Wilaya ya Hanang, Mwalimu Athumani Likeyekeye amewataka Walimu kujipanga kikamilifu ili kuipandisha halmashauri ya Wilaya ya Hanang kitaaluma kama alivyoelekeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu mwelekeo wa Serikali kielimu, wakati akizindua sera mpya ya elimu.
Mwalimu Likeyekeye ametoa wito huo leo alipokuwa mgeni rasmi katika kikao cha tathmini ya elimu ya awali na msingi kujadili hali ya ufaulu pamoja na upatikanaji wa chakula, kikao kilichowakutanisha walimu wakuu wa shule za msingi na maafisa elimu kata, kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri.
Amesema katika kuhakikisha Hanang inashika nafasi za juu kitaaluma, lazima kwanza walimu wajenge utamaduni wa kupeana motisha, walimu kuzingatia na kuhudhuria vipindi sanjari na kufuatilia maendeleo ya wanafunzi huku akiwaagiza wakuu wote wa shule kusimamia na kutekeleza mpango wa upatikanaji wa chakula shuleni.
Katibu Tawala wa wilaya ya Hanang Mwalimu Athuman Likeyekeye akizungumza na Wakuu wa shule za Msingi na Waratibu Elimu Kata, katika kikao cha tathmini ya elimu ya awali na msingi kilichofanyika Februari 26, 2025 (Picha na: Mwl. Carol Gisimoy)
Aidha, amewashauri walimu kujiendeleza kielimu ili waweze kuongeza maarifa na mbinu mbalimbali za ufundishaji ikiwa ni pamoja na kujiweka sehemu nzuri ya kupandishwa daraja. Na amewataka wakuu wa shule kuyasimamia mashamba ya shule yatumike kwa ajili ya matumizi ya shule na si kuyakodisha na au kuyagawa kwa watu binafsi.
Kwa upande wake, Afisa Elimu (Msingi) wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang Goefrey Abayo, amemhakikishia mgeni rasmi kuwa yeye pamoja na walimu watakwenda kuyatekeleza yote aliyoyaagiza na kushauri ili kuiweka Hanang katika nafasi za juu za ufaulu kimkoa na kitaifa.
Picha mbalmbali za washiriki wa kikao cha tathmini ya elimu ya awali na msingi kilichoketi kujadili hali ya ufaulu na upatikanaji wa chakula cha mchana shuleni, kilichowakutanisha walimu wakuu wa shule za msingi na maafisa elimu kata, kilichofanyika leo februari 26, 2025 katika ukumbi wa halmashauri. (Picha zote na; Mwl. Carol Gisimoy)
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: 0787821459
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.