Mkuu wa Wilaya ya Hanang’, Mheshimiwa Almishi Hazali, ameupokea jumla ya majiko banifu 1,583 ambayo yatauzwa kwa wananchi kwa bei ya ruzuku ili kuchochea matumizi ya nishati safi na kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa.
Majiko hayo yametolewa na kampuni ya L’S kwa ushirikiano na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) kama sehemu ya mpango wa kitaifa wa kuhamasisha nishati safi ya kupikia.
Akizungumza wakati wa kupokea majiko hayo, Mheshimiwa Hazali alisema kuwa serikali imelipia ruzuku ya asilimia 80, ambapo jiko moja lenye thamani ya Tsh 56,000 litauzwa kwa mwananchi kwa Tsh 11,200 pekee.
Ameongeza kuwa hatua hii inalenga kuboresha afya za wananchi, kupunguza uharibifu wa mazingira, na kuwawezesha wakazi wa vijijini kupata njia salama, nafuu na rafiki kwa mazingira ya kupikia.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: +255 762 362 950
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.