Wananchi wa vijiji mbalimbali wilayani Hanang wameungana kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani kwa kushiriki shughuli za usafi na ukusanyaji wa taka katika maeneo ya umma.
Maadhimisho hayo yameenda sambamba na kaulimbiu ya mwaka huu isemayo “Tunza Mazingira kwa kuzipa Taka Thamani”, ikilenga kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira na kubadili mtazamo kuhusu taka kuwa rasilimali yenye faida.
Katika tukio hilo lililoadhimishwa, Septemba 20, 2025 wananchi walijitokeza kwa wingi kusafisha barabara, masoko, maeneo ya taasisi na makazi, huku viongozi wa Halmashauri wakitoa wito kwa jamii kuendelea kuwa na utamaduni wa kulinda mazingira kila siku, badala ya kusubiri maadhimisho pekee.
Aidha, viongozi hao walisisitiza kuwa matumizi sahihi ya taka kama mbolea ya mboji, malighafi za viwandani au nishati mbadala yanaweza kusaidia kupunguza uchafuzi wa mazingira na kuchochea maendeleo endelevu.
Wananchi waliohudhuria walionesha mshikamano na kuahidi kuendeleza kampeni za mazingira katika maeneo yao kwa kushirikiana na halmashauri na wadau mbalimbali.
“Tunataka usafi wa mazingira uwe sehemu ya maisha ya kila siku. Hii siyo kazi ya serikali pekee, bali jukumu la kila mwananchi kuhakikisha maeneo yetu inabaki safi na salama kwa ajili ya afya za familia” alisema Martin Kirway mkazi wa Katesh.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: +255 762 362 950
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.