Wananchi wa vijiji mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Hanang wamejitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la usafi wa mazingira lililofanyika Jumamosi ya mwisho wa mwezi, likiwa na lengo la kuhakikisha usafi katika makazi, maeneo ya biashara na taasisi za umma.
Akizungumza baada ya zoezi hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang', Teresia Irafay, aliwapongeza wananchi kwa mwitikio wao mkubwa na kuwataka watendaji wa vijiji kuhakikisha wanasimamia kikamilifu utekelezaji wa zoezi hilo kila mwezi.
“Tunataka kuona kila kijiji kinashiriki ipasavyo kwenye Jumamosi ya usafi. Zoezi hili si la siku moja pekee, bali liwe sehemu ya maisha ya kila siku” alisema Irafay.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira wilaya ya Hanang', Ayubu Semdumbe, amesisitiza umuhimu wa wananchi wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katesh kukusanya taka zote katika sehemu rasmi ili kuwezesha gari la kukusanya taka kuyafikia maeneo yote kwa urahisi.
Amesema kwa sasa gari la taka huzunguka kila Jumamosi na Jumatano, katika kata ya Ganana na Katesh hivyo ni muhimu wananchi wa maeneo hayo wahakikishe taka zimehifadhiwa vizuri ili kulinda afya na usafi wa jamii.
Halmashauri ya Wilaya ya Hanang imekuwa ikitekeleza mpango wa kufanya usafi wa mazingira kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kwa kushirikisha wananchi wote, taasisi, na wadau wa maendeleo, ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuboresha afya ya jamii na kupendezesha miji na vijiji.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: +255 762 362 950
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.