Wananchi wa mji wa Katesh leo Oktoba 1, 2025 wamejitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ikiwemo barabara, makazi na maeneo ya umma.
Zoezi hilo ni sehemu ya utaratibu wa kawaida wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katesh, ambapo usafi wa jumla hufanyika mara mbili kwa wiki, Jumatano na Jumamosi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Teresia Irafay, amepongeza mwitikio wa wananchi kushiriki bila kushurutishwa na ameahidi kuendeleza utamaduni huo. Kwa mujibu Irafay, lengo ni kuufanya mji wa Katesh kuwa mfano wa kitaifa wa miji midogo yenye mazingira safi na yenye kuvutia.
Picha za wananchi na viongozi waliojitokeza kushiriki zoezi la usafi katika maeneo mbalimbali ya Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katesh. (Picha zote na: Mwalimu Carol Gisimoy, Hanang DC)
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: +255 762 362 950
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.