Wataalamu wa Afya wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang' wameendelea kutoa elimu juu ya ugonjwa wa M-pox ambapo leo timu ya Maafisa Afya imetoa elimu kuhusu ugonjwa huo katika shule ya sekondari Nangwa na chuo cha ufundi stadi (VETA), Nangwa.
Katika elimu hiyo, Dokta Catherine Amros amesema ugonjwa wa Mpox unaweza kuambukiza, kati ya mtu mmoja hadi mwingine kupitia majimaji ya mtu mwenye maambukizi na wakati mwingine kutoka kwenye vitu au maeneo yaliyoshikwa na mtu mwenye maambukizi ya M-pox.
Awali akielezea jinsi ugonjwa wa M-pox unavyoambukiza, Dkt. Erasto Mushi amesema ni ugonjwa hatari wa mlipuko unaosababishwa na kirusi kinachojulikana kama Monkeypox na kuwataka kila mwananchi kujilinda na ugonjwa huo.
Naye Dkt. Reuben Mangala wamebainisha dalili za ugonjwa huo kuwa ni pamoja na kupata upele, homa, vidonda kooni, maumivu ya kichwa, maumivu ya mgongo, uchovu mwilini, Kuvimba mitoki ya mwili.
Aidha, wataalamu hao wamebainisha baadhi ya njia za kujikinga na ugonjwa huo kuwa ni pamoja na kutosalimaina kwa kukumbatiana, kubusiana au kushikana mikono na mtu mwenye maambukizi, epuka kujamiana na mtu mwenye maambukizi ya ugonjwa huo, safisha na takasa sehemu zote na vitu ambavyo vinaguswa mara kwa mara.
Ikumbukwe, Machi 10, 2025 Serikali kupitia Wizara ya Afya ilitangaza kupokea wagonjwa wawili waliohisiwa kuwa na dalili za ugonjwa huo.
Hata hivyo, katika kudhibiti ugonjwa huo wilayani Hanang', mara tu taarifa ya uwepo wa visa hivyo kuripotiwa, wataalamu walianza kutoa elimu katika maeneo mbalimbali yenye mikusanyiko ikiwemo shuleni, nyumba za Ibada, minadani, kuandaa eneo maalum la kuwatenga washukiwa wa ugonjwa huo sanjari na kutoa mafunzo maalum kwa watumishi wa Afya 83 kutoka hospitali ya Wilaya Tumaini na wengine 34 kutoka Kituo cha Afya Katesh juu ya namna ya kukabiliana na ugonjwa huo.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: +255 762 362 950
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.