Mkuu wa Wilaya ya Hanang’, Mheshimiwa Almishi Hazali, ametoa karipio kali kwa watendaji wa kata 10 ambazo bado hazijaanzisha huduma ya chakula cha mchana kwa wanafunzi, akiwataka kuhakikisha huduma hiyo inaanza kutolewa mara moja.
Mheshimiwa Hazali amesema hayo leo Novemba 19, 2025 katika kikao cha tathmini ya lishe kwa robo ya kwanza ya mwaka 2025/26 na kuongeza kuwa suala la lishe ni msingi wa afya na ufaulu wa mwanafunzi, na hivyo halipaswi kuendeshwa kwa uzembe.
Katika kauli yake yenye msisitizo, Mheshimiwa Hazali alisema “Hili si suala la hiari. Kata nyingine zimeweza, kwa nini nyie mshindwe? Tafakarini kama kweli mnatosha kusimamia watoto wetu kupata lishe au mnahitaji kubadilika. Hatutavumilia uzembe unaowaumiza watoto.”

Aidha, amewaagiza watendaji hao kuandika barua za kujieleza, huku kikao kikiweka msimamo mpya kwamba kuanzia Januari 2026, mzazi atakayeshindwa kuchangia chakula cha mchana shuleni atatozwa faini ya shilingi 50,000, ili kuhakikisha hakuna mtoto anayesoma akiwa na njaa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’, Teresia Irafay, amesema kuwa ajenda ya lishe ni ya kudumu na halmashauri itaendelea kuongeza msukumo kwa shule zote, kuhakikisha kila mwanafunzi anapata mlo wa mchana.
Kikao hicho ni sehemu ya juhudi endelevu za serikali kuhakikisha afya, ukuaji na ufaulu wa wanafunzi vinaimarishwa kupitia huduma ya chakula shuleni.
MATUKIO KATIKA PICHA:







Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: +255 762 362 950
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.