Wananchi wa Wilaya ya Hanang' wamepokea Mwenge wa Uhuru chini ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2017, Ndg. Amour Hamad Amour
Ndg.Amour Hamad Amour. Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2017
MAJINA YA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU KITAIFA MWAKA 2017
"SHIRIKI KATIKA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YA NCHI YETU”
Mwenge wa Uhuru ukiwa Wilayani Hanang’ umekimbizwa Km. 161.3 ambapo umepita katika Tarafa 3 kati ya 5, Kata 8 kati ya 33 na Vijiji 10 kati ya 96. Jumla ya Miradi 7 imepitiwa na Mwenge wa Uhuru. Kati ya hiyo, Miradi 2 imezinduliwa, Miradi 3 imewekewa jiwe la msingi na miradi 2 imeonwa. Miradi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru ina thamani ya jumla ya Tshs. 897,367,849.76 ambapo kati ya fedha hizi, nguvu za wananchi ni Tshs.45,442,000.00, Halmashauri Tshs.34,214,958.00, wadau wa Maendeleo Tshs. 13,000,000.00 na Serikali kuu ni Tshs. 804,710,891.76
Uwekaji jiwe la msingi Madarasa 2 na ofisi 1 S/M Laja
Uwekaji wa jiwe la msingi Kituo cha Afya- Ishponga
Fuatilia taarifa fupi za miradi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru zilizowasilishwa kwa kiongozi wa mbio za mwenge mwaka 2017
Bofya hapa > TAARIFA YA MIRADI ILIYOPITIWA NA MWENGE 2017.pdf
Mkesha wa Mbio za Mwenge mwaka 2017 umefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Katesh A, na kuudhuriwa na Wananchi wengi kutoka viunga vyote vya Wilaya ya Hanang wakiongozwa na viongozi mbalimbali wakiwemo;- Wenyeviti wa Vijiji, Viongozi wa madhehebu ya dini, Viongozi wa mashirika ya Umma, Wawakilishi wa vyama vya Siasa (CCM, CHADEMA, CUF, ACT- Wazalendo, NCCR Mageuzi na TLP), Wakuu wa Idara na Vitengo vya Halmashauri, Mwenyekiti wa Halmashauri na Waheshimiwa madiwani, Kamati ya Ulinzi na Usalama(DED, DAS, OCD,DSO,Mshauri wa Mgambo, kamanda TAKUKURU, Afisa Magereza) wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya Bi. Sara Msafiri , ambapo asubuhi tarehe 11/09/2017 Mkuu wa Wilaya huyo aliukabidhi Mwenge wa Uhuru pamoja Viongozi wote wa Mbio za Mwenge 2017 kwa Mkuu wa Wilaya ya Babati Vijijini.
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: 0787821459
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.