Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Alexander Mnyeti ameanza ziara yake ya siku tano katika Wilaya ya Hanang. Lengo likiwa ni kuonana na Wananchi wote wa Wilaya ya Hanang', kufahamu kero zao na kuweza kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazokwamisha shughuli za kimaendeleo Wilayani hapo.
Mh. Alexander Mnyeti tarehe 12 Machi,2018 amekutana na Watumishi wa Makao Makuu ya Halmashauri, Walimu, pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali na kuweza kutoa hotuba sambamba na kutoa nafasi ya kufahama kero na changamoto mbalimbali kutoka kwa Watumishi na Viongozi hao na kuzipatia ufumbuzi papo kwa papo.
Katika Hotuba yake, Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh.Alexander Mnyeti amezungumzia mambo yafuatayo;-
Aliwataka Watumishi wote kutekeleza wajibu wao ipasavyo na kuhakikisha Ila ya Chama Tawala kilichoko madarakani (CCM) inatekelezwa ili kufanikisha Serikali ya awamu ya tano kufikia malengo yake.
Mkuu wa Mkoa amewataka Wakuu wote wa shule za sekondari kusimamia vyema ufundishaji wa wanafunzi mashuleni na kuhakikisha kwa mwaka 2018 kila shule inatimiza malengo ya ufaulu kwa asilimia 100% na hivyo kuinua kiwango cha elimu Wilayani Hanang. Aidha amewataka Wakuu wote wa shule za Sekondari pamoja na Maafisa Elimu Kata Wilayani Hanang watakaoshindwa kuondoa devision zero katika Kata na Shule zao basi wajiandae kuziachia nafasi zao kwani watakuwa hawatoshi.
Mkuu wa Mkoa ametoa rai kwa wananchi wote kuelimwishwa juu ya Sera ya Viwanda (Viwanda vidogo na viwanda vya kati) na kuwa Sera hii ni ya jamii na wananchi wote kwa ujumla hivyo kila mtu anapaswa kufahamu na kuitekeleza. Ameeleza kuwa Wilaya ya Hanang imepangiwa kuanzisha viwanda 15 jumla, aidha pasipo na ushirikishwaji wa kutosha kwa wananchi wa Wilaya ya Hanang pamoja na uwezeshwaji basi azma ya Serikali ya uwanzishwaji wa viwanda vidogo na viwanda vya kati hautatekelezeka. Mkuu wa Mkoa ameitaka ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa kushirikiana na ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi pamoja na wadau wote wa maendeleo juu ya Sera ya uanzishwaji wa viwanda vidogo.
Mh. Alexander Mnyeti ameeleza kuwa baadhi ya Wanasiasa wamekuwa wakwamishaji wa kubwa wa shughuli na utekelezaji wa Sera ya uanzishwaji wa viwanda vidogo katika Wilaya ya Hanang kwa ajili ya masilai yao binafsi. Mkuu huyo wa Mkoa ametoa onyo kali kwa Wanasiasa hao waache mara majo siasa hizo zinazokwamisha shughuli za kimaendeleo katika Wilaya ya Hanang. Aidha hatosita kuwachukulia hatua wakwamishaji wote wa utekelezaji wa Sera ya uanzishwaji wa viwanda na maendeleo ya wananchi kwa ujumla.
Mkuu wa Mkoa Mh. Alexander Mnyeti ameiagiza ofisi ya Mkuu wa Wilaya kusimamia migogoro yote inayotokea ndani ya Wilaya na migogoro hiyo kutafutiwa ufumbuzi mapema na kwa wakati ili Wilaya ya Hanang iondokane na Migogoro mingi isiyoisha. Aidha imeiagiza Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Hanang kutekeleza agizo hilo ndani ya mwezi mmoja na kukamilika
Mkuu wa Mkoa ameagiza Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Hanang kupeleka Wataalamu katika mashamba yanayomilikiwa na wawekezaji kwa ajili ya kufanya tathmini ya asilimia ya eneo la shamba linalotumika na wawekezaji hao. Aidha wawekezaji watakao bainika kutumia eneo la shamba chini ya asilimia iliyopangwa na Serikali basi mwekezaji huyo atanyang'anywa eneo hilo la shamba ama shamba zima.
Aidha Mkuu wa Mkoa Mh. Alexander Mnyeti ametoa ufafanuzi juu ya shamba la Bassotu ambapo aliwaomba wananchi kuendelea kuwa na subira hadi hapo maamuzi yatakapotolewa na ofisi ya Rais.
Mkuu wa Mkoa Manyara amesema Serikali ina mpango wa kutafuta mwekezaji mkubwa wa kuweza kuwekeza kiwanda kikubwa katika Mgodi wa Chumvi uliyoko Kata ya Gendabi Wilayani Hanang'. Mgodi huo kwasasa bado unachimbwa na wachimbaji wadogo wadogo wenyeji wa eneo hilo pasipo na vifaa maalumu vya uchimbaji na hivyo ubora wa chumvi hiyo kutoridhisha. Aidha Serikali inatarajia baada ya kupatikana kwa mwekezaji katika Mgodi huo wa chumvi, kiwanda hicho kitakuwa cha manufaa zaidi kwa jamii inayoizunguka na serikali kwa ujumla. Aidha Mgodi huo unatarajiwa kutoa ajira kwa vijana kati ya 800 hadi 1000 kipaumbele kikitolewa kwa wakazi wenyeji wanaozunguka eneo la Mgodi, kuongezeka kwa pato la Serikali, uboreshwaji wa huduma za kijamii na miundombinu mbalimbali na hasa katika eneo linalozungukwa na Mgodi huo.
Mh. Mkuu wa Mkoa alihitimisha hotuba yake kwa kutoa nafasi kwa Watumishi na Viongozi waliofika katika mkutano huo ili kutoa kero zao, changamoto na maoni yao kwa lengo la kuboresha na kuinua maendeleo ya Wilaya ya Hanang.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA TEHAMA
HALMASHAURI YA WILAYA YA HANANG
Email: ictsupport.hanangdc.go.tz
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: 0787821459
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.