Kwa niaba ya Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’, napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha kwa dhati kwenye tovuti yetu rasmi. Kupitia tovuti hii, tumedhamiria kuimarisha uwazi, uwajibikaji na utoaji wa taarifa kwa umma, kwa mujibu wa Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotoa haki ya kupata taarifa.
Tovuti hii ni jukwaa muhimu la kupata taarifa sahihi na za wakati kuhusu shughuli, mipango na maendeleo yanayotekelezwa na Halmashauri kwa manufaa ya wananchi wa Hanang’ na jamii kwa ujumla. Tunaamini kuwa upatikanaji huu wa taarifa utawasaidia wananchi kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya wilaya yetu.
Nawakaribisha kuitembelea tovuti hii mara kwa mara ili kufuatilia taarifa mbalimbali na kujifunza zaidi kuhusu huduma tunazotoa, mafanikio tuliyopata na fursa zilizopo. Maoni na ushauri wenu ni muhimu katika kuendelea kuboresha huduma zetu.
Karibuni sana.
Teresia A. Irafay,
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’
Hanang' District Council Headquater located at the Northern part of Katesh town in Ganana Ward
Postal Address: P.O Box 02 Katesh-Hanang'
Telephone: 027-2530022 / 42
Mobile: +255 762 362 950
Email: ded@hanangdc.go.tz
Copyright ©2016 GWF . All rights reserved.